Wednesday, July 14, 2010

Sir Edmund Hillary





Huyu ni mzungu wa kwanza kupanda mlima Everest mwaka 1953. Sababu kubwa yakuweka picha za huyu mtu nikutokana na funzo ambalo nimelipata toka kwake. Ukifuatilia kwa undani juu yake utagundua kwamba kupanda mlima mrefu kama Everest sio kitu kidogo, na chakushangaza ni kwamba awali alishindwa kabisa kuupanda, lakini alipojaribu kuupanda tena alifanikiwa.
Siku aliyokuwa anapokelewa Uingereza baada yakushindwa kupanda mlima Everest aliandaliwa Podium( ile sehemu yakuongelea kama mhubiri anapohubiria kanisani ni ndefu halafu vitabu au notisi zinakuwa juu yake), kuzunguka podium kulikuwa na picha nyingi zilizokuwa zinaonyesha mlima Everest.
Aki address watu waliopo, Sir Edmund aliangalia picha za mlima halafu akaongea maneno haya,"mlima everest, umenishinda mwanzo, lakini nakuhakikishia nitakushinda, kwani mim nakua lakini wewe haukui" mara ya pili alifanikiwa kupanda hadi kileleni.
Ni kweli kabisa ni wewe mwenyewe ndio unayejishinda kwani mlima haukui wala tatizo haliwi kubwa kama unavyofikiria, ila ukijipa nafasi yakutulia na kudili na hilo tatizo kwa hakika utalishinda. Siku zote fikiria positive juu ya kila negative situation.






muelimishaji2010

No comments:

Post a Comment