Wednesday, June 16, 2010

JE UNATAKA KUFANIKIWA?

ZIFUATAZO NI NJIA ZINAZOWEZA KUKUFANYA UFANIKIWE KTK MAISHA.

1. Associate with right people.

Hii ndio nguzo mojawapo itakayoweza kukufanya ufanikiwe, kwanza kabisa anza kujenga mahusiano na watu ambao wana uzoefu zaidi yako juu ya jambo ambalo wewe unataka likufanikishe iwe ni biashara au kazi fulani. Sidhani kama itakuwa busara kwa wewe unayetaka kuwa daktari bingwa ktk upasuaji uende kujihusisha na makundi ya wapiga debe au kukaa na mafundi gereji, watu wanatarajia kukuona wewe ukiwa karibu sana na watu walioko ktk field ya kitu unachokisomea au unachokifanya, hii itasaidia kukupa mwangaza na kukuonyesha changamoto ambazo utaweza kukutana nazo pmj na jinsi yakukabiliana nazo. Hivyo basi penda kukaa karibu na watu wenye ujuzi na waliofanikiwa zaidi yako ktk kitu unachotaka kukifanya ili ufanikiwe ktk maisha.

2. Be optimistic.

Hii ni hali yakuona jambo au kitu fulani ktk kufanikiwa kwake ijapokuwa waweza kuwa hujaanza kulifanya jambo husika. Ni hali yakuweza kuondoa mawazo mgando pmj na mawazo HASI ktk akili yako, kila jambo linapande mbili faida na hasara, Optimist ni mtu ambaye analiona jambo ktk faida zake na ktk kufanikiwa kwake, ni mtu ambae hakati tamaa kirahisi / kizembe na bila sababu za msingi, Albert Einstein ni mfano mzuri ktk hili, pia Watu hawa ni wale ambao kamwe hawawezi kupoteza FOCUS(mtazamo) ktk yale wayafanyayo ili wafanikiwe, pia ni watu ambao wako active muda wote ktk kupigania halali ya kile wakionacho kuwa kitafanikiwa. Kuwa mwenye mtazamo chanya muda wote kamwe usikubali kukatishwa tamaa na watu ambao hawafahamu dhati ya matamanio yako yakuona jambo ulitakalo likifanikiwa, hivyo jiamini na weka mtazamo wako sahihi muda wote. Ukijaribu kuangalia idadi ya matajiri na maskini duniani utagundua kuwa ni ndogo ikilinganishwa na ile ya maskini, sababu ni rahisi sana maskini waliowengi ni watu wenye mtazamo HASI ni watu ambao wamewekeza nguvu na akili zao ktk imani yakutowezekana kwa mambo wanayotaka yatokee mfano utakuta mtu anakwambia' tajiri niwe mimi? hiyo haitotokea' bila kufahamu kuwa maneno yanaumba. Hivyo basi wewe kama ni mtu unaetaka kufanikiwa ktk maisha yako jaribu kuwa n mtazamo sahihi pia jenga mahusiano mazuri kati yako na maneno au kauli uzitamkazo.

3. Don't be Excuside ( the ability to make excuse plans).

Sidhani kama huo msamiati nimeuweka sahihi, lakini kwa lugha nyepesi usipende kuwa mtu mwenye kutoa visingizio visivyo vya msingi pale unaposhindwa kutekeleza jambo fulani kwa wakati uliojipangia, weka mikakati chanya na siku zote weka mipaka ktk kuikamilisham, sababu au visingizio havitakufikisha popote, panga mambo yako ktk muda ulipjipangia kuyakamilisha. Naamini ktk dhati ya kwamba, kamwe humdanganyi mtu popote pale unapoona haja yakusema uongo ila kiukweli unajidanganya mwenyewe kwani siku zote unapoongopa ni wewe tu ndio unaejua kuwa umeongopa kwa upande wa pili inaonekana kuwa ulikiongea kina ukweli, hivyo upeka kutoa visingizio visivyo vya msingi pale unaposhindwa kutekeleza azma fulani au kuanza kupanga jinsi yakutoa visingizi, kwa hali hii hutofika popote.

4. Use time wisely( Productively).

Watu wanasema kuwa,time is always ripe to do what is right,according to Martin Luther King Jr,"time itself is neutral; it can be used either destructively or constructively",hivyo basi ukipangilia muda wako vizuri kila kitu utakifanya ndani ya muda uliojipangia, kimantiki kila mtu duniani kapewa zawadi ya masaa 24 ambayo hata Bill Gates na pesa alizonazo hawezi kununua masaa ya ziada, wachunguzi wa mambo waliwahi kutoa kanuni ndogo juu ya matumizi ya muda, walisema kuwa kwa siku kuna masaa 24, tukigawa haya masaa kwa 3, tutapata masaa 8,8,8(kwa maana kuwa kuna mafungu matatu ya masaa 8 nane), 8 ya kwanza ndio watu wanatumia ktk kulala ambacho ni kitu muhimu ktk maisha ya mwanadamu, 8 ya pili ndio watu hutumia makazini, shuleni au kwenye shughuli nyingine zakujenga taifa, 8 ya tatu ndio masaa ambayo yapo loose, hakuna kinachofanika ktk masaa haya, hapa wengi ndio muda wa kwenda saloon, kwenye misiba, vikao vya harusi au kufanya chochote nje ya masaa mengine kama nilivyotangulia kuyaonyesha, lakini swala la msingi lakujiuliza hapa ni kwanini wengine wanafanikiwa na wengine hawafanikiwi ktk maisha, tofauti ya matumizi ya muda ndio inayotufanya tusifanikiwe, Bakhressa hapewi masaa ya ziada wala Mengi hapewi masaa ya ziada, tofauti yetu kubwa ni kwenye matumizi ya masaa 8 ya tatu, kwani wengi muda huu tunautumia vibaya sana.
Watoa semina zakuleta hamasa wanasema kuwa kitu chochote ambacho ni kigumu kinapaswa kifanywe asubuhi kabla ya mambo yote (Eat thta Frog), unapoamka basi anza kufanya ile kazi ngumu kuliko zote ktk siku hiyo,hii inasaidia kupunguza kuchoka lakini pia asubuhi ni muda ambao mtu unaamka ukiwa na nguvu. Pia punguza muda wakuangalia Televisheni, moja yakiuongo kikuu ktk umaskini ni uangaliaji/utazamaji wa televisheni hususani kwa waafrika, tunapenda kuangalia Tv hata kwa vipindi visivyo vya msingi, kumbuka unapoangalia Tv wewe unakuwa unalimpa mtu mwingine kwa kila anachopenda huyo mtu kukifanya, Masanja Mkandamizaji ktk Ze Komedi show amekuwa akirudia mara nyingi kuwa, "wewe unacheka, sisi tunaingiza siku" hii ni kauli ambayo ukiichunguza kiundani ina maana kubwa, ktk nchi zilizoendelea Tv haiwekwi sebuleni, inachumba maalumu lakini kwetu Tv ipo sebuleni, kwa lugha za wenzetu Tv inaitwa IDIOT'S BOX kwa maana kwamba mjinga ndio anaeketi kuangalia Tv, wanasema Tv is a wonderful servant but a terrible master,kwa utafiti uliofanywa huko Ulaya ni kwamba matajiri hutazama Tv masaa 5 kwa wiki na wanachoangalia mara nyingi ni habari za kiuchumi, lakini hali ni kinyume kwa maskini kwani wao hutazama Tv masaa 7 na dk 15 kwa siku, jaribu kuona hiyo tofauti halafu useme kuwa matajiri Mungu kawapendelea, Tv is the biggest time waster.

5. Read Books.

Wanasema,there are only two things that are going to change your life; 1. the people you meet and 2. the books you read. Hivyo basi jenga tabia yakujisomea vitabu vingi kadri uwezavyo kwani kuna elimu kubwa sana ambayo inapatikana katika vitabu, bwana mmoja Jim Rhon aliwahi kusema, "read everything''. Rafiki yangu Dizzo aliwahi kuniambia siku moja kuwa vitabu ni marafiki ambao hujawahi kukuonana nao akimaanisha kwamba waandishi wa vitabu ni marafiki zako au wageni ambao wamekutembelea nyumbani kwako, pengine yawezekana hao watu ungeweza kukutana nao kwenye ndege au mabasi lakini kupitia vitabu umeweza kuwakaribisha hadi nyumbani kwako. Kuna elimu kubwa sana inayopatikana ktk vitabu tofauti na ya darasani, hivyo ukitaka kufanikiwa jaribu kusoma vitabu tofauti tofauti uone jinsi ideas za wenzako zilivyo.

6. Plan

Weka mipango ambayo itakubidi uifanyie kazi kila uamkapo, na jitoe zaidi juu ya malengo yako ambayo unataka kuyatimiza, usijionee huruma kwani kisichokuua kitakukomaza kiaskari, tofauti kubwa kati ya tajiri na maskini ni kwamba tajiri anaweka mipaka ya maumivu yake, kwamba, ngoja niumie kwa muda huu halafu baada ya hapa nianze kula matunda ya maumivu yangu, lakini hii imekuwa kinyume na maskini ambaye tangu anazaliwa hajiwekei mipaka ya maumivu yake, yeye ni kuumia tu kila kukicha hadi anaingia kaburini. Weka malengo yako leo, ni nini hasa unataka kukikamilisha na jiwekee mipaka au deadline, lakini pia settle the map kwa ajili yakuona utapita wapi na wapi ktk kuyafikia malengo yako, pia malengo yenyewe yawe makubwa ila sio makubwa sana yasije yakakuumiza sana mbeleni. Wanasema, To fail to plan, is to plan fail.

7. Focus.

Direction is more important than Speed. Hii nimeongelea kidogo hapo juu ktk kuwa optimistic lakini ni muhimu sana kwa mtu kutopoteza mwelekeo wake, kwa chochote ulichopanga kukitimiza jaribu kuweka konsetresheni kwacho, usiwe mtu wakurukia mambo, leo umeshika hili, kesho unashika lile, focus on your goals and move with your plans, katika hili usikubali kuyumbishwa na watu wasiojua ukubwa wa ndoto yako(malengo) hivyo shikilia ktk naweza yako na uone mwisho utakuaje.

8. Do what you resolve to do.

Fanya kile unachotakiwa kukifanya ktk muda unaotakiwa kukifanya, penda kuwa na kiherehere cha kukamilisha mambo yako kwa wakati uliojipangia, kwa style hii lazima utafanikiwa, usiwe mtu wakupostpone vitu,siku zote kesho haijawahi kuonekana, je wewe umewahi kuiona kesho? kwani kesho ya jana si ndio leo?, tomorrow shall never come and it has never been there, so don't procrastinate bcoz in two days tomorrow will be yesterday. Fanya unalotakiwa kufanya na sio unalojisikia kufanya, hivi ndivyo matajiri walivyo ukiwafuatisha ni lazima utafanikiwa.

9. Count your blessings.

Time is always of the essence when one counts hi/her blessings. Kwa tafsiri rahisi ktk hili ni kwamba jipongeze kwa hatua yoyote ndogo uliyoifikia, kwa kufanya hivi itakupa hamasa yakukamilisha hatua kubwa uliyojiwekea, Sappa See nabulee...., whatever you have no matter how small, it counts ( Kihaiti hicho), hivyo basi jipongeze kwa hatua uliyopiga na pia weka nidhamu ktk kupongeza hata watendaji wako. Siku zote kumbuka wajibu wako.

10. Mind your own business ( MYOB).

Jali na thamini kile unachokifanya,usikurupuke ktk kuweka tamaa yakujihusisha na vitu ambavyo vipo nje ya mipango na malengo yako, kuwa na wivu wakumaliza mambo yako kwanza ndipo uhangaike na mambo mengine, thamini muda wako na majukumu yako ktk kukamilisha malengo yako.

Mwisho kabisa, thamini afya yako kwani bila hiyo kamwe hutofanya lolote, kuwa na tamaa yakujiona mzima muda wote, play by the rules, heshimu jamii yako na weka dhati ya mapenzi yako kwa Mungu.






muelimishaji2009

No comments:

Post a Comment