Napenda kuongea/kuandika machache juu ya kichwa cha habari hapo juu.
Ni wazi kwamba ni wachache sana ambao wanaweza kulijibu swali langu hapo juu kwa ufasaha, pia ni wengi watakaoweza kunijibu kuwa wanayapa maisha tafsiri juu ya mambo yanayowatokea(we treat life according to the events that happens. Ila kwa ujumla maisha yanatafsiri pana sana, na kila mtu anweza kuyapa tafsiri yake.
Kwa upande wangu mimi naamini kuwa tafsiri ya maisha imebebwa na yote niyafanyayo mimi, kwangu mweneywe na kwa wengine kadhalika na yale wanifanyiayo watu wengine aidha mazuri au mabaya.
Wengine huenda mbali nakuamini maisha ni kuishi vizuri tu, lakini je maisha haya yakuishi vizuri yanaletwa na nani/ serikali au mtu mwenyewe? ni swali gumu wengi huamini kuwa serikali ndicho chombo chenye mamlaka yakuyafanya maisha yawe mazuri, hawaamini kuwa sio mambo yanayowatokea bali ni vile wanavyoyakabili yanayowatokea ndio kipimo pekee cha ugumu au uzuri wa maisha yao, kwani yanayotokea yanatokea kwa kila mtu, jaribu kuvuta kumbukumbu juu ya tukio la mtikisiko wa uchumi ambao kila mwanadamu lilimgusa, lakini kuna walioathirika zaidi na wengine hawakuathiriwa kwa kiasi kikubwa. Kwa lugha nyepesi ya ufafanuzi juu ya hili ni kwamba, wale walioathiriwa zaidi walikuwa na approach mbaya juu ya tatizo lililowakabili na wale walioathiriwa kidogo walikuwa na approach nzuri juu ya tatizo.
Motivational Speaker mmoja(Jim Rhon marehemu) ambaye mimi binafsi namkubali sana, aliwahi kusema sio upepo wa bahari ndio utakao determine mwelekeo wako bali ni jinsi wewe ulivyoseti ngalawa yako(it is not the blow of the wind but the setting of the sail that determines your destination).
Kwenye hili kama tukirudi nyuma kwenye tatizo la mtikisiko wa uchumi, watu wengi walipoteza ajira zao, na hili ni tatizo kwani wengi wameegemeza hatma ya maisha yao kwenye kazi zao, bila kuamka nakufikiria kuwa hakuna Future kwenye kazi, Future ipo kwa yule anaemiliki hiyo kazi na mara nyingi sio mwajiriwa bali ni mwajri wako, wengine wanatumia kazi walizonazo kuwanyanyasa wahitaji wa huduma hizo. Nakumbuka siku moja rafiki yangu Raphael Chima aliwahi kuonywa na Mama yake mzazi mbele yangu kuwa be Good to people when you go up coz you will meet them when you come down. Hii ni kweli kabisa, wengi wetu tunatumia vyeo vyetu bila dhamana, lakini ikikumbukwe kuwa maskini wa leo ndio tajiri wa kesho na pengine tajiri wa leo ndio maskini wa kesho, hivyo tuwe makini tusijifanye miungu watu.
Zaidi ya yote maisha ni kutoa, saidia pale inapohitajika mwanafalsa mmoja aliwahi we are richer when we give and poorer when we keep, ni kweli huwezi kupata kupata ni lazima utoe ndio upate, hayati Bob Marley naye aliwahi kusema kuwa, in this world you give your more to receive your less, hivi ndivyo maisha yalivyo, ikumbukwe inasemekana kuwa Mungu hakuumba tajir na maskini lakini hata hivyo hakuna aliezaliwa na nguo wote tulizaliwa uchi, hii inaamanisha kuwa kuhangaika kwa kila mmoja wetu ndiko kuna mfanya mtu awe zaidi ya mwingine kiuwezo lakini inasikikitisha pale mtu mwingine anapotumia jasho la mwingine ktk kujinufaisha inauma sana(chukulia mfano wa EPA).
Lakini naomba pia nije kwa hawa wahitaji misaada, kwa imani yangu ni watu ambao hawajiwezi, sasa swali linakuja hapa kuwa mtu asiejiweza ni yupi? kwani kuna wengine kwa mtazamo tu wanaonekan wanajiweza lakini utawakuta barabarani wanaomba misaada badala yakutafuta shughuli yeyote ya halali nakuifanya, ni bora mtu umsaidie maarifa yakujikwamua kuliko kumpa msaada ambao ndani yake umefanyiwa kazi toka kwa mtu ambae tayari amejikwamua, ndugu zangu vilema na wengine wanaopretend kuwa ni vilema, ikukumbukwe bwana mmoja(Motivational Speaker based in Kenya, Pepe Minambo) kwenye kitabu chake cha be inspired b4 you expire alisema, Disability is not inability, kwa maana kwamba hata kilema anaweza kufanya kazi na akarekebisha sehemu fulani ya maisha yake.
Upendo ni ngao yenye muhimu
Mwisho kabisa napenda kuwaasa watu juu ya umuhimu wakuthamini maisha, na kila kukicha kila mtu ajitahidi kuwa bora zaidi ya jana, wengi wetu tunachukulia kuiona siku mpya ni kama halali yetu bila kufikiria kuwa Mungu baba amekuwa na upendo wa pekee juu yetu hadi akaruhusu tuione siku mpya, yawezekana ili tufanye marekebisho ya makosa tuliyoyafanya jana, ila imekuwa kinyume, mwingine anaomba aione kesho ili alipize kisasi juu ya baya alilotendewa jana, mwingine ndio anapanga akavamie sehemu ili aweze kujipatia pesa kwa njia isiyo ya halali, mwingine anaomba aione kesho ili atimizie azma yake yakutembea na mke wa mtu pamoja na mabaya mengine mengi, sasa je ni yupi anapaswa kupewa zawadi ya siku ya kesho? huyu anayefikiria visasi, kutembea na mke wa mtu , anayefikiria kukaba na kuua au huyu anae omba kuiona kesho ili akamilishe jambo fulani au ikibidi aende kumuomba masamaha aliyemkosea akiamini kuwa kukosa kwake kumemuweka mbali na bwana? Tumeonywa juu ya mambo mengi lakini tumekuwa na kiburi juu maisha yetu wenyewe. Jaribu kufikiria wewe mvuta sigara au mlevi kupindukia ni lipi bora kunywa bia 4 kwa siku ambazo gharama yake ni zaidi Tsh 6000 au kula papai pamoja na ndizi mbivu chache ambazo gharama yake haifiki Tsh 2000 kwa siku? Lakini cha ajabu mtu huacha kula matunda lakini anaweza kunywa hata bia za Tsh 8000 kwa siku na hii pengine ndiyo ratiba yake ya kila siku, je kuna aliewahi kwenda hospitali akashauriwa anywe pombe? Au mara nyingi tuendapo hospitali pamoja na dawa tunazopewa bado Daktari anatushauri tule matunda na maji kwa wingi. Mabadiliko ni hatua na sio kwa siku moja mtu anaweza kuacha tabia yake, wachina wana msemo wao kuwa, it is easier to reshape a mountain or a course of a river than a person’s character, lakini je kuna aliezaliwa na tabia mbaya aliyonayo?
Jali maisha na thamini uhai wako, zingatia au fuata kanuni zote muhimu, kuna vitu rahisi ambavyo vipo ktk uwezo wa kila mtu kuvitekeleza lakini inashangaza watu wengi hawazingatii, wazungu wanamsemo wao kuwa, things easy to do are the things easy not to do, utakuta mwingine anavuka barabara kwa maringo utadhani anaundugu na magari ijapokuwa magari hayo yanapita kwa kasi ya ajabu mno, mtu kama huyu akigongwa atalaumu dereva? Kuna kanuni nyingi na sheria nyingi ambazo zinapuuzwa kila kukicha lakini hatima yake ni madhara makubwa, jaribu kufikiria magari yaendayo mikoani, kila basi linapaswa kuwa na mikanda ktk siti ya kila abiria na abiria wanaaswa juu yakufunguka mikanda hiyo ili kujiweka ktk mazingira yapunguzayo uwezekano wakupata athari kubwa pengine kama ajali itatokea, lakini chakushangaza pamoja na jitihada hizi baadhi ya abiria kufunga mkanda kwao ni kama mwiko haijalishi ni mara ngapi anasafiri, sasa mtu kama huyu gari/basi likipinduka akachomoza nje nakujibamiza kwenye jiwe akafa kuna haja yakumlilia? hata kisheria mtu huyu wanamuhusisha na kitu kinachoitwa Contributory Negligence kama ataamua kupeleka kesi mahakamani incase kama hajafa au familia yake ikiamua kufanya hivyo, sheria inamuweka ktk nafasi yakuchangia sehemu ya janga alilolipata. Ndugu zangu ni ktk kuziheshimu sheria ndogo ndogo na kanuni ndogo ndogo ndipo twaweza heshimu zile kubwa.
Kifo chako chaweza kuwa chanzo cha matatizo ya wengi utakaowaacha, hivyo kuwa makini, thamini uhai wako, sambaza upendo, jiamini kwani ni wewe tu ndio unaejua uwezo ulionao, fahamu kuwa wewe niwathamani
Yapende maisha na Jipende wewe mwenyewe kabla ya yote.
muelimishaji2009
No comments:
Post a Comment