Thursday, June 17, 2010

HOW BIG IS YOUR DREAM?.......

Are you longing to have this kind of a House?
Or, you are after having a lovely family?
Is this kind of a House you're dreaming of?
My dream Car


Swali la kwenye title hapo juu ni rahisi lakini pia ni gumu kama tu wewe ni mtu unaeishi ktk malengo uliyojipangia.
Wapo watu wenye kutamani kuishi vizuri, kuwa na gari zuri au hata familia bora lakini chakushangaza watu hawa hawaishi ndani ya malengo yao.
Lakini pia wataalamu wanasema kuwa, kama malengo yako hayajawahi kukuamsha usiku wa manane na kuyafikiria basi malengo yako ni madogo mno ambayo hayahitaji nguvu ktk kuyakamilisha.
Je wewe una malengo gani ktk maisha?
Bwana mmoja mwandishi wa vitabu na pia ni motivational speaker, Pepe Minambo katika kitabu chake cha Be Inspired Before you Expire anasema kuwa; the most tragedy in life is not death, but life, the life that has not achieved its purpose and potential. Hii ni kweli kabisa kwani jaribu kufikiria leo hii wewe ukifa utakumbukwa kwa lipi hasa? au jaribu kufikiria leo hii wewe unakufa lakini familia yako ina vitu vyakumbukumbu juu yako, achilia mbali watoto, fikiria kama kuna kiasi kikubwa cha pesa kwenye akaunti au una Asset tofauti tofauti sehemu mbalimbali, hii si kheri kwako wewe uliekufa na kwa wale wanaobaki?
Mtu anaeishi bila malengo ni sawa sawa na msafiri asiyejua anapoelekea, hivyo basi weka malengo yako leo na yaandike pia ili yakupe hamasa yakuyafanyia kazi, lakini kingine cha msingi ni lazima malengo hayo yawe makubwa (shoot for the moon). Pia yatamke malengo yako au yaweke sehemu ambayo yataonekana na watu wengine, hii itakupa wewe hamasa yakuyafanyia kazi kila kukicha, ishi ktk tamaa yakutaka malengo yatimie na si vinginevyo, waepuke wote wanaokukatisha tamaa kwani ni wewe tu ndie unaejua siri na njaa ya malengo uliyojiwekea, hakuna kinachoshindikana chini ya jua, Sky is always the limit, penda kuweka plan kwa ajili yakufanikisha malengo yako na ikibidi yavunje vunje ktk udogo wake ili kupiga hatua moja yakukamilisha lengo dogo kutakupa hamasa yakulifikia lengo kubwa kwa wakati.
Jaribu kufanya kitu tofauti pindi uanapo kuwa malengo yako hayafanikiwi, kwa maana kwamba kama ulikuwa umeweka matarajio yako ktk mshahara ndio ukamilishe malengo yako na muda unaenda halafu malengo hayafikiwi basi angalia mbinu nyingine, usibadilishe malengo yako kwa sababu tu huyafikii kwa wakati, kinachotakiwa kubadilika ni fikra pamoja na plan yakuyafikia, wanasema, "if you do what you have always done, you will get what you have always got" hivyo basi angalia njia nyingine mbadala ambayo ni ya halali.
Japokuwa matatizo yatakuwa mengi ktk kuyafikia malengo yako, hii isiwe sababu ya wewe kukata tamaa, kwani wanasema, problems are success in disguise, hata mimi nakubaliana na hili kwa asilimia mia moja kwani kila tatizo linalokupata lina chembe ya mafanikio ndani yake, bwana mmoja wa Kimarekani ambaye ni motivationa speaker, Chris Widener, anasema kuwa, when God wants to send you a gift, he wraps it up with a problem, when he wants to send you a big gift, he wraps it up with a big problem. Lakini chakushangaza wengi wetu tunahangaika zaidi na kasha lililofungiwa zawadi husika ambalo kasha lenyewe ndio tatizo badala yakuhangaika na zawadi ynewe iliyopo ndani, na siku zote zawadi inakuwa ni somo ambalo unatakiwa kujifunza kutokana na tatizo husika.
Be optimist kama unataka kukamilisha malengo yako, epukana kabisa na mawazo mgando( mawazo Hasi) ambayo yatahatarisha kufanikiwa kwa malengo yako, jiweke mbali na Dream killers, wale watu wanaotaka kuua ndoto/malengo yako.
Thamini muda wako uliyojipangia katika kukamilisha mambo yako, usikubali kuingiliwa kwa ratiba yako na mambo yasiyohusiana.

Range Rover vogue.
Hii ni gari ya ndoto yangu, popote ninapoiona huwa napatwa na goosebumps, nafanya kila niwezalo kuhakikisha kuwa nakuja miliki hili gari ktk maisha yangu, though i can't count my days bcoz i have got fewer days ahead than behind but atleast God's Power may grant me some more days forward towards accomplishing my burning desire to own this byutiful baby. Naamini ktk mipango yangu kwenye kufanikisha azma yangu na pia nafanya wajibu wangu kila siku ktk hili.

Kama kuna kitu unachotaka kukikamilisha na unahisi kuwa your conscious won't be at peace with yourself bila kukamilisha hilo lengo basi anza kulifanyia kazi sasa, weka mikakati thabiti yakufanikisha azma yako, according to Pepe Minambo, every person born in this world has a purpose and for every purpose there is a God given potential to fulfill it. So determine what's yo purpose today na anza kuifanyia kazi. Hakuna linaloshindikana hata kama ndoto yako ni kubwa kiasi gani, because impossible is the vocabulary that exists only in a fool's dictionary.

Huu ni muda muafaka wa wewe kutambua thamani yako, u bora sana wewe na u wa thamani ya juu sana, usijione hufahi na wala usijishushe thamani yako because God didn't waste his time in creating Nobody, so you are always somebody.
Kubali kuumia kwa ajili ya thamani yako na thamani ya malengo uliyojiwekea, kubali hata kudharaulika ikibidi kwani mwishoni atakayefurahia matunda ya majasho yako ni wewe mwenyewe.

***Make your life itself a creative work of ART***









No comments:

Post a Comment