Friday, February 12, 2010

UTAFITI: MA"BABY FACE" HUISHI MAISHA MAREFU ZAIDI


Sote tunawafahamu. Wengine ni wanablogu wenzetu. Japo wana umri mkubwa lakini nyuso zao zinaonekana kuwa za kitoto. Hata wanapotuambia umri wao hatuwaamini na tunawabishia kwa sababu wanaonekana wangali vijana na kamwe hawalinganishiki na wenzao wanaodai kuwa nao sawa kiumri. Nyuso zao huwa zimetakata na ngozi zao nyororo zisizo na doa la chunusi wala mwonekano wa kuzongwa na maisha daima huonekana kung’ara. Huwa tunawaita ma“baby face”. Kwa Kisukuma watu hawa huitwa “bagidanamhala” kama ni wanaume au “bagidagiguluha” kama ni wanawake.Katika utafiti uliofanywa nchini Denmark, wanasayansi wamethibitisha kwamba ma“baby face” huishi maisha marefu zaidi kuliko wenzao wenye nyuso zilizokomaa. Utafiti huu ulijumuisha jozi za mapacha wapatao 1,800 wenye umri unaozidi miaka sabini. Baada ya kuwapiga picha nyuso zao, makundi matatu ya watu tofauti tofauti ambao hawakujua umri sahihi wa mapacha hawa waliombwa kukadiria umri wao. Baada ya miaka saba, mapacha walioainishwa kama ma“baby face” ndiyo walikuwa wakiendelea kuishi kwa wingi ikilinganishwa na wenzao wenye nyuso zilizoakisi umri wao kwa usahihi; na matokeo haya hayakuathiriwa na jinsia wala mazingira. Kwa hivyo, wanahitimisha wanasayansi hawa, kuwa na uso wa “kitoto” kunahusiana moja kwa moja na kuishi maisha marefu., maelezo zaidi,http/matondo.blogspot.com

Pichani ni mwanamuziki Kenneth Edmond(Baby face),ana umri wa miaka 51







muelimishaji2009

2 comments:

  1. http://matondo.blogspot.com/2009/12/utafiti-mababy-face-huishi-maisha.html

    ReplyDelete
  2. Dogo, naona umedesa kila kitu kutoka hapa

    http://matondo.blogspot.com/2009/12/utafiti-mababy-face-huishi-maisha.html

    Huwezi kutoa japo vidokezo vyako na mawazo yako mwenyewe kuhusu jambo hili? Kama hii ishu imekuvutia - why? Mbona umeiweka hapa? Just copying and pasting for no apparent reason(s)???

    This goes to show that education ya Tanzania ni choka mbaya and we are just producing watu wa kudesa - no critical thinkers!!! Kind of sad!

    ReplyDelete